Michezo

Leroy Sane aondolewa kwenye kikosi cha Ujerumani 

Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim  Low amewashitua wapenzi wa soka baada ya kumtoa kwenye kikosi cha wachezaji 23 Winga hatari wa Manchester City, Leroy Sane hii leo ikiwa ni harakati za kujiweka sawa kuelekea michuano ya kombe la Dunia nchini Urusi.

Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim  Low

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter Shirikisho la soka la Ujerumani limethibitisha kuachana na mchezaji huyo mchanga zikiwa zimebaki siku chache kabla ya mtanange wa kombe la Dunia kuanza nchini Urusi.

Winga hatari wa Manchester City, Leroy Sane

Mapema mwaka huu, Sane ametwaa tuzo ya mchezaji mdogo wa kulipwa wa mwaka ligi kuu ya nchini Uingereza (PFA) akiwa anaitumikia klabu yake ya Manchester City.

Kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents