Michezo

Leroy Sane aihofia klabu hii kwenye mbio za Ubingwa ligi kuu England

Leroy Sane aihofia klabu hii kwenye mbio za Ubingwa ligi kuu England

Winga wa klabu ya Manchester City na taifa la Ujerumani Leroy Sane amefanya mahojiano na kituo cha sky sport baada ya mazoezi wakati wa maandalizi ya ligi kuu nchini Uingereza ambayo inatarajiwa kuanza mapema mwezi August mwaka huu.

Sane amesema kuwa maandalizi yanaenda vizuri na wamejiandaa vya kutosha kuanza msimu mpya wa ligi 2018/19.Ikumbukwe kuwa Manchester City wako nchini Marekani wakijiweka sana kwa ajili ya msimu mpya na tayari wamecheza baadhi ya michezo ukiwemo mchezo wa juzi dhidi ya Dortmund na kupoteza mchezo huo kwa kufungwa goli moja likipatikana kwa mkwaju wa penati.

Katika mahojiano hayo sana amezungumzia vitu mbalimbali hasa kuhusiana na usajili wa Riyad Mahrez aliyesajiwa kutoka Leicester City inayoshiriki ligi kuu nchini humo na kusema kuwa inahitajika nguvu ya ziada ya kupambana ili kupata namba katika kikosi hicho cha Guardiola.

Lakini pia maeongelea kuhusiana na tuzo yake aliyoshinda mwishoni mwa ligi ya mchezaji bora chipukizi baada ya kuulizwa,Je! kuhusu kuitetea tuzo hiyo Sane alisema kuwa “Inawezekana sana ila anahitaji kupambana vya kutosha tena kuongeza nguvu ya ziada kucheza vizuri ili kushawishi kupigiwa kura tena.

Baada ya kuulizwa kuwa ni timu gani anahisi italeta upinzani mkubwa katika mbio za kuwania Ubingwa,Sane alisema “Nahisi Chelsea watafanya vizuri sana kutokana na kocha waliomsajili maana sisi tulicheza na Napoli katika michuano ya UEFA na tulipata shida sana kushinda nahisi ni kwa ajili ya kocha wao Maurizio Sarri” lakini pia Liverpool watakuwa vizuri pia.

Winga huyo Mjerumani alichaguliwa kuwa mchezaji bora chipukizi katika ligi kuu nchini Uingereza akiwashinda Rashfod wa Manchester United,Delle Alli wa Totenham na wengineo wengi.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents