Habari

Leseni mpya za udereva kuunganishwa kwenye kompyuta

NAIBU wa Usalama wa Rais,Mohamed Aboud, amesema kuwa, serikali inakusudia kutoa leseni mpya za udereva zilizounganishwa katika mtandao wa kompyuta, ili kudhiti madereva wazembe na ajali za barabarani.

Na Mwandishi Wa Mwananchi


NAIBU wa Usalama wa Rais,Mohamed Aboud, amesema kuwa, serikali inakusudia kutoa leseni mpya za udereva zilizounganishwa katika mtandao wa kompyuta, ili kudhiti madereva wazembe na ajali za barabarani.


Aboud alisema kuwa kwa utaratibu huo, madereva wote watalazimika kupata mafunzo maalum kabla ya kupata leseni hizo na kudhibiti za kughushi.


Mapema aliliambia bunge kuwa, kiko cha Usalama wa Barabarani, kimeanzisha Kitengo cha elimu kwa lengo la kutoa elimu kwa watumiaji wote wa barabara katika shule za msingi na sekondari.


Mpango huo, ni miongoni mwa hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa na serikali kukabiliana


na ajali za barabarani.


Takwimu za mwaka 2005 na 2006, zimeonyesha kuwa ajali za barabarani zimeongezeka kutokana na leseni za kughushi na uelewa mdogo wa watumiaji wa barabara juu ya sheria za usalama barabarani, ubovu wa magari, uzembe wa madereva, ubovu wa barabara na mwendo kasi.


Mbali na kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara, serikali imetoa maelekezo kwa Jeshi la Polisi kukamata magari mabovu na kuyachukulia hatua za kisheria.


Vilevile imeweka vituo vya kukagua ratiba za mabasi zinazotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Baharini nchini (Sumatra), ili kudhibiti mwendo kasi.


Jeshi la Polisi limetakiwa kusimamia vizuri faini za papo kwa papo na kuwafikisha mahakamani wanaofanya makosa na kuweka kumbukumbu za makosa ya usalama barabarani.


” Serikali itaendelea kuzifanyia ukarabati sehemu korofi katika barabara zote na kuweka alama za usalama barabarani na Jeshi la Polisi litaendelea kufanya doria katika barabara kuu ili kuyakamata magari yote yanayokiuka sheria za usalama barabarani,” alisema.


Maelezo hayo yalitokana na swali la Mbunge wa Magogoni, Mohamed Ali Said aliyetaka kujua ni hatua gani za makusudi zitakazochukuliwa na serikali kuondoa tatizo hilo.


Source: Mwananchi

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents