Mapenzi

Let’s talk about sex: G-Nako akiri kulipenda mno tendo hilo la kuongezea wanadamu duniani

Sio kitu cha kushangaza tena ukikuta msichana ananyanyua simu na kumpigia kijana kumtaka kimapenzi. Wala haishangazi kukuta kijana ana wapenzi zaidi ya mmoja na pengine wote wanajuana kwenye mzunguko huo.

Wala sio “surprise” tena kukuta vijana wamekaa kistoni, wakizungumza na kuchambua aina za mahusiano waliyonayo, kuanzia yale ya mbio fupi, mchepuko, friends with benefits na wakati mwingine mwenye wengi ndio kinara.

Ndio maana msanii G-Nako kutoka Weusi na yeye alipoulizwa na DJ Tee, mtangazaji wa kipindi cha Shujaaz Radio Show kuhusu ni kundi gani kati ya vijana wa kike na kiume ambalo hufikiria sex zaidi katika michakato yao ya kila siku, aliamua kufungua roho kuhusu hili.

Huku akijifikiria kwa umakini, G-Nako alisema hawezi kusema kwa uhakika kwamba ni jinsia gani inapenda sex zaidi ya nyingine. “It depends na mtu na mtu, kwa mfano kama mimi hapa napenda sex sana” alisema mkali huyu wa Go Low.

Katika mjadala mkali wenye mihemko ya kutosha uliofanywa na wasanii wa muziki wa Bongo Fleva wa kundi la Madada Sita wakiwa na vijana wengine, wasichana walisikika wakiwatuhumu wavulana kwa kupenda sex zaidi ya wanawake na wavulana wakijaribu kutoa kila sababu za kuonesha kwamba wasichana ndio wanaendekeza zaidi kamchezo hako. Msanii Lizzy wa kundi hilo lenye maskani yake TMK, alisema kwamba ingawa msichana anaweza kuwa na wanaume zaidi ya mmoja haimaanishi anakusudia kufanya nao mapenzi wote.

Alitolea mfano kwamba msichana anaweza kuwa na bwana kwa ajili ya mavazi, mwingine kwa chakula, na mwingine kwa kumnunulia vifaa vya urembo na mwingine kwa ajili ya kufanya nae mapenzi tu. “Ikitokea mwanaume anaanza kuniambia tufanye sex na akiendelea kusisitiza nitamuacha” alisema mmoja wa wasanii hao wa Madada Sita

Akijaribu kuwatetea wanaume katika mjadala huo, Walter ambaye ni mmoja kati ya Managers wasaidizi wa kundi hili linalokuja kwa kasi na ngoma yao ya “Matobo” alisema kwamba wanawake ndio hupenda kufikiria sex zaidi kwa kuwa hata mtaani wanawake ndio hujiuza zaidi ya wanaume. Kauli hii ya Walter ilifanya ashambuliwe kwa maneno na akina dada hao huku wakisema kwamba siku hizi kuna wanaume wengi tu ambao wanajiuza pia na wanajulikana kwa jina maarufu kama Marioo, hivyo sio akina dada pekee yao wanaobadilisha ngono kwa pesa.

Mtaalamu wa afya kutoka katika chuo kikuu cha Dar es salaam Dr. Tuholani alitoa ufahamu wake kwa kusema kwamba suala la kupenda kufanya sex ni jambo la kisaikolojia na linaweza kuwa pande zote. “nilikuwa na rafiki yangu wakati tukiwa shule akasema hakuwa anapenda kufanya mapenzi na mwanaume kwa sababu aliwahi kubakwa akiwa na miaka 11, jambo lililomharibu kisaikolojia na kuwachukia wanaume” alisema Dr Tuholani akizungumzia majibu aliyopewa na rafiki yake huyo.

Hata hivyo DR. Tuholani alisema kuwa wanawake mara nyingi huwa na vipaumbele vingi vinavyoweza kuwafanya wasifikirie mapenzi tofauti na ilivyo kwa wanaume.

Tafiti zilizochapishwa na mitandao wa ell/msnbc.com zinasema asilimia 66 ya wanaume walioko kwenye mahusiano wanapata hamu ya kufanya mapenzi tofauti na asilimia 25 ambayo ni wanawake.

Sex ni moja kati ya basic needs katika maisha ya wanadamu na baadhi ya viumbe, japokuwa hutegemea na hali ya mazingira yanayoweza kusukuma hamu ya kuhitaji au kutohitaji tendo hilo. Je wewe unaonaje? Wanawake ndio huendekeza Sex zaidi ya wanaume?

Imeandikwa na: Irene Robinson na Abdul Mbwambo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents