Videos

‘Let’s Wait’ na video ya ‘Utanifanya Nighairi’ zampaisha Cindy Rulz kimataifa

Wiki hii na wiki iliyopita zimekuwa za mafanikio makubwa kwa rapper wa kike wa Tanzania Corrinne Mary aka Cindy Rulz.

artworks-000061529704-hkyq0w-t500x500

Wimbo wake mpya, ‘Let’s Wait’ aliomshirikisha producer Dunga, si tu umepokelewa vizuri nchini, bali hata kwenye blogs za Marekani. Blog ya kwanza iliyokubali uwezo wa rapper huyo aliye chini ya studio ya Fish Crub, inaitwa Death Chamberz Music ambao wamesema pamoja na kutoelewa baadhi ya maneno ya Kiswahili kwenye wimbo huo, bado wamevutiwa na kila kitu walichokisikia kwenye Let’s Wait.

“A female rapper from Tanzania who is rapping in a multiple languages really intrigued me. Don’t really understand everything that is said but she certainly has great delivery. This seems to be a pop tune if you listen to the beat and the singing hook. Gives me and old school hip head vibe on her style But still feminem. Love her track Redio,” wameandika.

Kupitia Twitter pia waliandika: @CindyRulz music is a true musical language don’t have to know what you’re saying to understand one love keep sending material.”

[soundcloud url=”https://api.soundcloud.com/tracks/117920064″ width=”100%” height=”166″ iframe=”true” /]

Blog nyingine iliyopokea vizuri ngoma hiyo ni Grime Culture.

Katika hatua nyingine, mtandao maarufu wa Rap Genius umemhakiki msanii huyo.

Kama haitoshi, video ya wimbo wake, Utanifanya Nighairi iliyotoka wiki hii imewekwa kwenye mtandao wa Marekani, Viewhiphop.com

Huo unaonekana kuwa mwanzo tu ya mafanikio kwa rapper huyu wa kike, mengi yanakuja zaidi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents