Burudani

Lewis Hamilton aopoa mrembo mpya

Dereva mahiri wa magari ya Mercedes kutoka Uingereza, Lewis Hamilton aliyeshindwa kuwakilisha vizuri timu yake katika mashindano ya Formula 1 mjini Monaco ameamua kupoza machungu kwa kuopoa mrembo mpya.

Jumatatu hii Hamilton ameonekana akila bata katika fukwe za Cannes villa zilizopo kwenye mji wa Monaco nchini Ufaransa na mwanamitindo Bella Hadid ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa muimbaji The Weeknd.

Bella hajawahi kuonekana na mpenzi mpya tangu alipoachana na muimbaji huyo wa Marekani, naye Hamilton amekuwa akionekana mewenyewe sehemu mbalimbali tangu alipoachana na ex wake Nicole Scherzinger.


Lewis na Nicole enzi za mapenzi yao

Cannes villa kwa sasa ndio sehemu inayoonekana kutembelewa zaidi na mastaa mbalimbali akiwemo Scott Disick na mpenzi wake Sofia, Koutney Kardashian ambaye alitembelea eneo hilo mwenyewe pamoja na wengine.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents