Michezo

Lewis Hamilton atwaa taji la Mexico Grand Prix

Dereva wa magari ya mashindano ya Langa Langa kutoka Mercedes, Lewis Carl Davidson Hamilton amefanikiwa kushinda taji lake la nne la dunia.


Lewis Hamilton (wa katikati) wakiwa na Sebastian Vettel (wa kwanza kulia)

Hamilton ameshinda taji hilo la Mexico Grand Prix licha ya kumaliza akiwa katika nafasi ya tisa baada kugongana na dereva wa Ujerumani, Sebastian Vettel kutoka kampuni ya Ferrari.


Lewis Hamilton akishangilia baada ya kushinda michuano ya Mexico Grand Prix

Lewis anakuwa dereva wa kwanza kutoka nchini Uingereza ambaye amefanikiwa zaidi katika mchezo huo na kufanikiwa kuvunja rekodi ya mkongwe wa michuano hiyo Sir John Young ‘Jackie’ Stewart ambaye amewahi kushinda mataji ya Italian Grand Pix (1965) na German Grand Pix (1973).

Kwa sasa Hamilton anaungana na madereva wengine kama Vettel na Alain Prost wa Ufaransa ambao wamefanikiwa kushinda mataji manne kila mmoja ya mchezo huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents