Habari

LHRC yaiomba serikali kuondoa adhabu ya kifo

Kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC kimeiomba serikali kuondoa adhabu ya kifo kutokana na adhabu hiyo kuenda kinyume na haki za binadamu na kuathiri kiasi kikubwa haki za msingi ya kuishi.

img_9496

Akitao tamko juu ya siku ya maadhimisho ya kupinga adhabu ya kifo duniani ,mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho Dk Hellen Kijo Bisimba amesema adhabu ya kifo imekuwa kinyume na siyo sahihi.

“Adhabu hii inakuwa kama ya kulipiza kisasi,kwasababu haimsaidii yule aliyekufa zaidi ya kuongeza mtu mwingine kufa, hata ndugu wanaosema ndugu yetu amekufa akiuawa huyo aliyeuwa wao hawampati tena ndugu yao kwahiyo haisaidii,” alisema.

“Lakini pia utafiti haujaweza kutuonyesha kwamba adhabu hii imesaidia kuondoa hilo tatizo,” aliongeza Bisimba.

Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimekuwa zikishinikizwa na mashirika ya kimataifa hasa yale ya utetezi wa haki za binadamu kufuta sheria hiyo.

Machi 6 mwaka huu Kamishna wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay alinukuliwa kupitia Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) akilaani kuendelea kwa adhabu hiyo alioyoiita kuwa ni ‘ukatili dhidi ya binadamu.’

Zaidi ya watu 360 wanasubiri adhabu hiyo nchini.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents