Fahamu

Lifahamu jalala kubwa zaidi nchini China lililojaa kabla ya muda uliopangwa – Video

Lifahamu jalala kubwa zaidi nchini China lililojaa kabla ya muda uliopangwa - Video

Jalala kubwa kabisa la takataka nchini China linaelezwa kujaa, miaka 25 kabla ya muda uliopangwa. Jalala hilo lililo katika jimbo la Shaanxi, lenye ukubwa wa sawa na viwanja 100 vya mpira wa miguu, lilijengwa kupokea tani 2,500 kwa siku.

Lakini badala yake lilikuwa likipokea tani 10,000 za takataka kwa siku, kiasi kikubwa kuliko jalala jingine lolote nchini humo.

China ni moja ya nchi zinazofanya uchafuzi wa mazingira zaidi duniani, na imekuwa ikihangaika kwa muda mrefu kutatua changamoto zinazozalishwa na watu bilioni 1.4 wa nchini humo.

Jalala kubwa la Jiangcungou lililo kwenye mji wa Xi’an lilijengwa mwaka 1994 kwa lengo la kufanya kazi mpaka mwaka 2044.

Jalala hilo linawahudumia zaidi ya watu milioni nane.Lina ukubwa wa karibu mita za mraba 700,000, na kina cha mita 150 na uwezo wa mita za ujazo milioni 34.

Mpaka hivi karibuni, Xi’an ni moja kati ya miji michache nchini China ambao kwa kiasi kikubwa inategemea jalala hilo kupokea uchafu kutoka majumbani, hali iliyosababisha kujaa haraka.

Mwanzoni mwa mwezi huu, mfumo wa kuteketeza takataka ulifunguliwa na mingine takribani minne zaidi inatarajiwa kufunguliwa mwaka 2020. kwa pamoja mifumo hiyo inatarajiwa kuteketeza takataka kiasi cha tani 12,750 kwa siku.

Hatu hii ni sehemu ya mpango wa taifa kupunguza idadi ya majalala, na badala yake kutumia njia ya kuziteketeza takataka.

China huzalisha takataka kwa kiasi gani?

Mwaka 2017, China ilikusanya tani milioni 215 za takataka zinazotoka majumbani, kwa mujibu wa takwimu za nchini humo, ambacho ni kiwango kilichoongezeka kutoka tani 152 miaka kumi iliyopita.

Nchi hiyo ilikuwa maeneo ya majalala 654 na maneo 286 ya kuteketeza takataka.

Haifahamiki kwa kiasi gani China huchakata taka kwa ajili ya matumizi mengine, kwa kuwa hakuna takwimu zilizotolewa.China ina mpango wa kuchakata 35% ya takataka katika miji mikubwa mwishoni mwa mwaka 2020 kwa mujibu wa ripoti ya serikali.

Mwezi Julai, mpango wa kuchakata takataka ulitangazwa kuwa wa lazima mjini Shanghai, hatu iliyoleta ”taharuki” miongoni mwa wakazi.

Mwaka 2015,kulitokea maporomoko katika jalala la takataka kusini mwa mji wa Shenzhen, na kusababisha vifo ya watu 73.

Jalala liliundwa kutunza takataka kwa ujazo wa mita za mraba milioni nne, rundo la takataka lenye urefu wa mita 95.

takataka
Image captionTakataka za plastiki mjini Kuala Langat

China inapokea takataka kutoka nchi nyingine?

Haifanyi hivyo hivi sasa, ilikuwa inafanya hivyo zamani mpaka mwishoni mwa mwaka 2017 ikaamua kupiga marufuku uingizaji wa takataka za madaraja 24 tofauti.

Mwaka 2017 pekee, China ilipokea tani milioni saba za takataka za plastiki kutoka Ulaya, Japan na Marekani na tani milioni 27 za takataka za makaratasi.

Nchi nyingine, kama Malaysia, Uturuki, Ufilipino na Indonesia imepunguza pia.

Baadhi ya nchi hizi zimepiga marufuku kuingizwa kwa aina fulani za takataka wakati mwingine hata kuzirudisha zinakotoka.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents