Michezo
Ligi kuu England kuendelea wikiendi hii
Ligi kuu ya Nchini England kuendelea tena wikiendi hii kwa michezo kadhaa, Jumamosi Norwich itaikaribisha Sunderland, Everton wao watakuwa wenyeji wa Southampton, Man Utd watakuwa wenyeji wa Aston Villa katika dimba la Old Traford , Newcastlle itamenyana na Swansea city, West Brom watawaalika Watford na Chelsea watakuwa darajani Stamford dhidi ya Manchester City.
Jumapili Vinara wa ligi Leicester city watakuwa nyumbani na West Ham,Bournemouthwatawaalika Liverpool na Arsenal itamenyana na Crystal Palace.