Michezo
Ligi kuu ya Soka la England kuendelea tena wikiendi hii
Ligi kuu ya Soka ya England inataendelea tena Wikiendi hii baada ya kupisha michuano ya FA CUP ambapo Jumamosi patakuwa na michezo mbalimbali.
Vinara wa ligi hiyo Leicester city itapambana na Norwich city, Southampton na Chelsea, Stoke na Aston Villa, Watford na Bournemouth, West Brom na Crystal Palace, West Ham itaikaribisha Sunderland.
Ligi hiyo itaendelea tena Jumapili kwa michezo miwili Manchester united watakuwa wenyeji wa Arsenal uwanja wa Old Traford, na Tottenham wakiwakaribisha Swansea city, Liverpool itachuana na Everton,New castlle watakuwa wenyeji wa Manchester city.