Michezo

Ligi ya mpira wa kikapu kuzinduliwa Dar

Shirikisho la Mpira wa Kikapu ( NBA) litazindua rasmi msimu wa kwanza wa ligi ya mpira wa kikapu kwa vijana kwenye kituo cha vijana cha Michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete jijini Dar es Salaam mnamo tarehe 27 Februari mwaka huu.
basketball1

Sherehe hii ya ufunguzi wa mashindano hayo itahudhuriwa na mchezaji nyota wa mchezo huo na mwandamizi wa Shirikisho la mpira wa Kikapu Ulimwenguni Allison Feaster utakuwa ni uzinduzi rasmi wa ligi ya Mpira wa Kikapu kwa Vijana wenye umri kati ya miaka 12 na 14.

Ligi hii itajumuisha shule zipatazo thelathini (30) kutoka maeneo ya karibu na kila shule ikiwakilisha moja wapo ya timu 30 zinazoshiriki Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Marekani.

Ligi ya mpira wa kikapu ya vijana (Jr. NBA League) ni ligi ya NBA ya dunia inayoshirikisha mchezo wa mpira wa kikapu kwa vijana, wavulana kwa wasichana na inafundisha stadi za msingi za mchezo wa mpira wa kikapu pamoja na maadili muhimu ya mpira wa kikapu kwa wachezaji wanaoanza, Lengo likiwa ni kusaidia kukuza na kuboresha uzoefu wa Wachezaji, Makocha na Wazazi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents