Michezo

Ligi ya Wanawake ya sogezwa mbele

Ligi kuu ya Wanawake ya shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) hatua ya 6 Bora ambayo ilikuwa ianze Febrauri 18, 2017 Uwanja wa Karume, imesogezwa mbele kwa muda wa juma moja.

Ligi hiyo sasa itaanza rasmi Februari 26, 2017 kwenye uwanja huohuo wa kumbukumbu ya Karume, Ilala mahali zilipo ofisi za TFF. Hii ni kutokana na sababu ambazo ziko nje ya uwezo wetu.

Timu sita zilizofanikiwa kufika hatua ya Sita Bora ni JKT Queens ya Dar es Salaam, Mlandizi Queens ya Pwani na Fair Play ya Tanga kutoka Kundi “A” wakati kutoka Kundi “B” zimo Marsh Acedemy ya Mwanza, Sisterz ya Kigoma na Panama ya Iringa.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, kutakuwa na mechi mbili kila siku katika kituo kimoja kwa mujibu wa kanuni. Kituo hicho ni Uwanja wa Karume, ulioko Ilala jijini Dar es Salaam ambako mchezo wa kwanza utaanza saa 8.00 mchana wakati mwingine utaanza saa 10.00 jioni.

Ratiba mpya inaonesha kwamba siku ya Februari 26, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya JKT Queens na Mlandizi saa 8.00 mchana wakati saa 10.00 kutakuwa na mchezo kati ya Fair Play na Sisterz.

Ratiba kamili kwa mechi inazofuata itatolewa wiki ijayo. Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza au unaoweza kujitokeza kutokana na mabadiliko hayo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents