Like Father Like Daughter au?

Imekuwa ikiaminika kuwa Dully Sykes ni mmoja kati ya wasanii ambao wamekuwa na vibweka vya aina yake katika medani ya muziki na maisha ya kawaida ya wasanii, lakini pamoja na hayo kijana huyu ameamua kuyakabili majukumu pamoja na kuangalia future

Dully na Misky


 


Imekuwa ikiaminika kuwa msanii Dully Sykes ni mmoja kati ya wasanii ambao wamekuwa na vibweka vya aina yake katika medani ya muziki wa kizazi kipya na hata katika maisha ya kawaida ya wasanii, lakini pamoja na hayo unaweza kuona jinsi kijana huyu ambavyo amebadilika na kuamua kuyakabili majukumu pamoja na kuangalia future yake kwa ujumla.


 


Akizungumza na Mwandishi wa bongo5.com alisema kuwa hivi sasa amekuwa makini sana katika kumuandalia mtoto mazingira mazuri hivyo ana kila sababu ya kuwa mchapa kazi zaidi ili kuhakikisha mtoto wake wa kike ajulikanaye kwa jina la Misky Sykes.


 


Dully ambaye anamiliki studio inayokwenda kwa jina la Dhahabu Records iliyopo maeneo ya Tabata, na hivi karibuni yuko katika hatua za mwisho kukamilisha albam yake ambayo makeke yake yameanza kuonekana katika singo yake abayo inaendele kufanya vizuri katika chati za muziki wa kizazi kipya hapa nchini.


 


Alikutana na mwandishi wa bongo5.com katika pita pita zake huko town ambapo Dully Sykes alikuwa ameambatana na Mama wa mtoto wake Bi Fatma Said akiwa na Binti yake huyo ambaye ukimtazama unaweza kuona nae ana dalili za kuwa supa staa wa aina yoyote na sio lazima awe msanii kama alivyokuwa Baba yake.


 


Dully na Wife 


 


“Sitashangaa sana kuona mwanangu nae anafuata nyendo zangu isipokuwa itabidi niwe makini sana katika kumuelekeza kilichokuwa kibaya na kilichokuwa kizuri ili aweze kukuwa katika malezi yaliyokuwa bora, naweza kuona kuwa mimi binafsi nimekuwa mtu mzima sana kwani napa hisia za kuwa mwenye majukumu jambo ambalo linanifanya nimshukuru sana Mungu” alisema Dully Sykes.


 


Star huyu amewahi kutamba na hits kibao ambazo zimemuwezesha kuwa juu na jina lake kubaki katika ramani ya muziki hapa nchini mpaka hivi sasa.



Bofya hapa kutembelea sehemu ya video na kuangalia baadhi ya nyimbo zake

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents