Likizo Tyme Waongeza Wasaanii

Wasanii wa muziki wa Reggae na Dancehall kutoka Kingston Jamaica Tanya Stephens na Tento Mento & Devonte wameongezwa katika listi ya wasanii watakaotumbuiza katika tmasha la Likizo Tyme.

Wasanii wa muziki wa Reggae na Dancehall kutoka Kingston Jamaica Tanya Stephens na Tento Mento & Devonte wameongezwa katika listi ya wasanii watakaotumbuiza katika tmasha la Likizo Tyme.

Akizungumza na waandishi ya habari leo katika ukumbi wa klabu ya Maisha Oysterbay jijini Dar-Es-Salaam,mkurugenzi wa kampuni ya Entertainment Masters Bibi Helen Sweya amesema wasanii hao wanakuja kuongeza nguvu wasanii wawili wa Boyz 11 Men na Joe Thomas ambao walitangazwa awali.

Akiendelea mama Sweya alisema hii ni kutokana na wao kutaka kuridhisha marika yote ya umri ambayo yanapenda kula burudani hapa nchini ambapo muziki wa taratibu yaani R&B unapendwa na watu wazima wakati ule wa Reggae na Dancehall unapendwa zaidi na Vijana.

Akichangia Katika maelezo ya mama Sweya meneja wa kitengo cha muzikina masula  ya ufundi bwana Francis Ciza almaarufu kama Dj majizo amesema  shoo hiyo itakuwa ni ya wasanii wa kutoka nje pekee ili kuwapa watanzania burudani waliyoikosa kwa muda mrefu.

Wasanii wote wanatarajiwa kuwasili siku ya tarehe 3 Desemba na kisha kwenda kampala tarehe nne ambapo watatambulishwa na kisha kurudi Dar-Es-Salaam tarehe 5 mabapo watapiga shoo hiyo

Viingilio vimepangwa kuwa V V I P 100,000 ukinunua tiketi kabla na 120,000 getini, V I P 60,000 ukinunua tiketi kabla na 70,000 getini. Kawaida kiingilio ni shiling 30,000 kwa watakaonunua tiketi kabla na 40,000 getini.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents