Burudani

Lil Wayne alazwa hospitali mara mbili ndani ya saa 24

Rapper Lil Wayne amelazwa tena hospitali baada ya kupata tatizo lingine linalofanana na alilolipata akiwa kwenye ndege binafsi.

Mwanzilishi huyo wa Young Money Entertainment alikuwa amesharuhusiwa kutoka hospitali jana kutokana na kupatwa na dalili za kifafa.

Weezy alikuwa kwenye ndege akitokea Texas kuelekea Los Angeles wakati tukio la pili lilipotokea baada ya kuanza tena safari iliyokuwa imekatishwa kwa muda.

Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Weezy alilazwa kwa mara ya pili kwenye hospitali iliyopo Louisiana.

Juzi Lil Wayne alipelekwa kwenye hospitali ya huko Texas baada ya kupatwa dalili hizo akiwa kwenye private jet kiasi cha kumfanya atue kwa dharura.

Lil Wayne, aka Dwayne Carter Jr. yupo busy na maandalizi ya albam yake mpya “I Am Not a Human Being II,” itakayotoka December.

Pia ameandika kitabu cha historia yake kiitwacho “Gone Till November.” Kinachohusiana na miezi nane aliyokaa kwenye gereza la Rikers Island kwa kosa la kumiliki silaha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents