Burudani

Lil Wayne aruhusiwa kutoka hospitali

Baada ya kuwa ICU kwa siku 6 katika hospitali ya Cedars-Sinai Medical Center ya huko West Hollywood, hatimaye Lil Wayne ameruhusiwa kutoka hospitali baada ya kupata nafuu.

img-lil-wayne-cover_17135846584

Taarifa hizo zimetolewa na Mack Mane wa YMCMB kupitia Twitter:

MACK MANE

Vyanzo vya karibu na Weezy vimedai kuwa bado ni dhaifu lakini walau anaendelea vizuri na anapanga kukaa kimpya mpaka atakapopona vyema.

Katika hatua nyingine, Birdman amelazimika kuzikanusha tetesi kuwa tatizo lililopelekea Wayne alazwe ni madawa.

“It didn’t have nothing to do with drugs, “Birdman alimwambia Angie Martinez wa Hot 97. “Hakuna kitu kama hicho. Kwangu ndivyo anavyofanya kazi. Anafanya kazi mchana na usiku, ni mpambanaji tu kwenye muziki. Lakini haikuwa sababu ya madawa. Anahitaji tu muda wa kupumzika. Atarejea kawaida kama mtu mwingine yeyote.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents