Burudani

Lil Wayne kumburuza mahakamani aliyevujisha Carter V

By  | 

Rapa Lil Wayne anatarajia kumshitaki mmiliki wa kampuni ya usambazaji muziki mtandanoni ya MSMB inayomilikiwa na Martine Shkreli kwa kuvujisha kopi kadhaa za nyimbo zitakazokuwepo kwenye album ya “Tha Carter V”.

Mwanasheria wa Wayne kwa kushirikiana na Kampuni ya Universal Music wote wameamua kumfungulia kesi Shkreli kwa kuvujisha mdundo(tune) ambazo zinapatiakana katika album ya “Tha Carter V’ itakayo toka ndani ya huu mwaka 2017.

Tune ya kwanza ya Album ya “Tha Carter V” iliachiwa kupitia njia ya mtandao mnamo mwaka jana wakati wa sikukuu ya Krismas, lakini Wayne hakumshitaki Shkreli kutokana na kujiapiza kutorudia kosa hilo tena. Hata hivyo Shkreli hakuishia kuvujisha ngoma tu tha Wayne kwani miezi mitano kabla aliripotiwa kuvujisha ngoma 2, za wasanii wengine akiwemo Kendrick Lamar.

Chanzo cha karibu cha Wayne kimesema kuwa Shkreli anafanya hivyo ili aweze kupata kiki kwa watu lakini sasa atajutia anachofanya kwani atashitakiwa.

Na Laila Sued

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments