Bongo5 ExclusivesVideos

Lilian Internet apewa sh milioni 5! Mashujaa wawatia tumbo joto wamiliki wengine! [Video]

[youtube]http://www.youtube.com/watch?v=9m2hvloh9kM[/youtube] Kiongozi wa Bendi ya Mashujaa Music, Jadol FFU amesema mikakati ya kuongeza wasanii katika bendi yao bado inaendelea lengo likiwa ni kuimarisha bendi hiyo. Jadol alipoulizwa kuhusiana bendi hiyo kuchukua wasanii wa sehemu moja alisema na kuhusu mvutano wa nani hasa anayemfuata mwenzake alisema kati ya msanii na uongozi wa bendi hiyo, alisema kazi yake ni kujua msanii gani wanamtaka baada ya hapo jambo hilo analifikisha kwenye uongozi na ndipo wanalifanyia kazi.

Aidha amedai kwa sasa wanampango wa kuwaongeza wanenguaji, jambo ambalo limefanya bendi nyingi kuingia kwenye hofu ya wanenguaji wao, kutokana na bendi hiyo kutoa donge Nono.

[youtube]http://www.youtube.com/watch?v=BmLcDbH4kiE[/youtube] Mmoja wa wanengauji wa bendi ya Twanga Pepeta Lilian Internet, alisema alifuatwa na Chaz Baba ilikuungana na Bendi ya Mashujaa na kukubali, kutokana kugewa donge nono la sh milioni tano, kupangishiwa nyumba pamoja na mshahara mnono. Amesema yeye yupo zaidi kimaslahi, na kujifunza mengi zaidi kwenye muziki.

[youtube]http://www.youtube.com/watch?v=0d36QxrYiLY[/youtube] Wakati huo mpiga gitaa la solo na benzi katika bendi ya Twanga, Ally Akida naye alisema alifuatwa na viongozi wa bendi hiyo akati akiwa mapumziko, na kuahidiwa maslahi makubwa na hivi sasa anasubiri kuona mkataba wake.

Ally Akida amesema yeye bado hajasaini mkataba wowote na bendi hiyo, hivyo hawezi kusema kama yeye ni mwanamuziki wa Mashujaaa, na kama akisaini basi atahakikisha lazima apeleke barua kwenye bendi yake ya Zamani ya Twanga Pepeta.

Tembelea hapa kuangalia mahojano zaidi kati ya bongo5 na Lilian Internet na Ally Akida.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents