Burudani

Dully Sykes ndiye chimbuko la Sharobaro

Imedokezwa kuwa msanii wa Bongo Fleva, Dully Sykes ndiye mwanzilishi wa neno maarufu miongoni mwa vijana, Sharobaro lakini yeye mwenywe hajui alipolitoa.

Muimbaji Hakeem 5 ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa katika mazungumzo na Dully Sykes pamoja Bob Junior, ndipo ilitokea Dully akawaita Sharobaro kutokana walikuwa wanapendeza sana.

“Lilimtoka tu sijui mwenye kalitoa wapi, Bob Junior akaniambia lakini hili jina limekaa kinyamwezi, nikamwambia naliona limekaa vizuri, tukawa tunapenda kulitumia kwa sababu lina swagger,” amesema Hakeem 5.

Ameongeza kuwa Bob Junior alisafiri na kwenda India na aliporejea na kufungua studio ndipo waliposhauriana studio hiyo waipe jina la Sharobaro.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents