Burudani

Linah na Rachel wajibu kuhusu kukopi ngoma ya Vanessa na Maua

By  | 

Ikiwa ni siku chache zimepita tangu Linah na Rachel watoe ngoma yao mpya ‘Same Boy’, wamekanusha ngoma hiyo kukopi idea kutoka kwenye ngoma ya Vanessa Mdee na Maua Sama ‘Bounce’.

Linah ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa ngoma yao ina idea tofauti na ile ya kina Vanessa na isitoshe ngoma hiyo ilikuwepo kabla Bounce haijatoka.

“Hii yetu tunazungumzia ile kwamba kwa pamoja tunamtaka mwanaume mmoja lakini ile yao inaelezea wapo na huyo mwanaume lakini hawajuani, sisi ni watu ambao tunajuana,” amesema Linah.

Same Boy ni ngoma ya pili kwa Linah na Rachel kukutana katika ngoma moja baada ya kushirikishwa na kundi la Makomando katika ngoma yao inayokwenda kwa jina la Chap Chap.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments