Habari

Lindi:Watu zaidi ya 4500 wakosa Makazi kufuatia Mvua kubwa iliyonyesha

Zaidi ya Wananchi 4500 wa Vijiji Sita, Wilayani Kilwa hawana mahala pa kuishi baada ya nyumba zao kusombwa na maji kutokana na mvua kubwa iliyonyesha kwa siku tatu mfululizo Mkoani humo

Mkuu wa Wilaya hiyo, Christopher Ngubiagai amevitaja Vijiji hivyo kuwa ni Kilanjelanje, Nanjirinji A Ruatwe, Njinjo, Nakiu na Nanjirinji B. Amesema mbali na nyumba kubomoka, mashamba na mifugo ya wananchi hao nayo imesombwa na maji

Timu ya uokoaji imekwenda eneo lililokumbwa na mafuriko kwa boti kunusuru maisha ya Wananchi na watapelekwa katika maeneo yaliyotengwa. Amewataka watu wa kada mbalimbali kutoa msaada kwa Wananchi hao

“Tunaendelea kuwaokoa na kuwapeleka maeneo ambayo tumeyatenga. Tunahitaji msaada wa chakula, dawa, nguo na vitu vingine muhimu,” amesema Ngubiagai

Na Jacquiline Ngoya

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents