Burudani

Linex afunguka sababu za ukimya wake

Msanii Linex amefunguka na kusema ukimya wake kwenye muziki unasababishwa na yeye kuamua kujipa mapumziko kwani alifanya kazi kwa miaka saba bila kumpumzika.

Linex

Linex amesema licha yeye kuwa kimya hakuna mtu anaweza kumzuia kufanya muziki jinsi yeye anavyotaka au kuchukua nafasi yake kwa sababu muziki anaofanya yeye ni wa kipekee.

“Kwa hiyo ninaweza kurudi muda wowote, sisemi kuwa nitakaa muda mrefu bila kutoa wimbo kwa sababu kuna vitu nilitakiwa kuvifanya lakini sikuvifanya ambavyo ni mapumziko, nimefanya kazi zaidi ya miaka saba sijawahi kukaa nyumbani hata siku mmoja,” Linex amekiambia kipindi cha Twenzetu na kuongeza.

“Kwa hiyo nimejipa mapumziko huu ni mwezi karibia wannne sasa, nimekaa nyumbani nimepumzika, nimeandika kazi, kwa hiyo any time nitafanya kitu ambacho ni kikubwa,” amesema Linex.

By Peter Akaro      

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents