Tia Kitu. Pata Vituuz!

Linex: Mzungu (ex girlfriend) ndiye mwanamke pekee maishani mwangu niliyemkuta na ‘bikira’

Unakumbuka Linex aliwahi kuwa na uhusiano na binti wa kizungu miaka kadhaa iliyopita hadi akafikia hatua ya kumvisha pete, lakini baadae uchumba ukayeyuka? Hit maker huyo wa ‘Aifola’ ametaja utofauti wa msichana huyo na wasichana wengine wote aliowahi kushea nao ‘tunda’.

Linex

Linex amesema kuwa msichana huyo raia wa Finland ndiye msichana pekee aliywahi kumkuta hajaguswa na mwanaume yeyote (bikira) kati ya wote aliowahi kuwa na uhusiano nao kimapenzi.

“Unajua nchi za ukanda ule wa Scandnavia wanawake wanajitunza sana, na mzungu ndiye mwanamke pekee maishani mwangu niliyemkuta na ‘bikira’” alisema Linex kwenye kipindi cha Hatua tatu cha Times Fm.

Ameongeza kuwa mawsiliano kati yake na binti huyo ambaye alirudi nchini kwao yalikuwa yanaendelea licha ya kuwa hawako pamoja hadi majuzi alipoona picha mitandaoni za kilichodhaniwa kuwa ndoa ya Linex wakati wa kutambulisha wimbo mpya ‘Kwa Hela’, kitendo kilichomfanya binti huyo pia kuamini kweli Linex ameoa.

Chanzo: Times Fm

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW