Tupo Nawe

Linex – sikuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu ila sasa nishampata

Linex ambaye picha ya cover ya ngoma yake mpya ‘Kwa Hela’ ilizua utata kwa kufanya wengi waamini kuwa amefunga kufunga ndoa, amesema sasa yupo kwenye uhusiano baada ya kuwa single kwa kwa muda mrefu.

linex

“mimi nina muda mrefu actually sikua kwenye mahusiano na mtu yeyote lakini nowdays nipo kwenye mahusiano na mtu,” alisema Linex kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio.

Linex bado hajaamua kumtaja hadharani mpenzi wake wa sasa.

Mwaka 2014 Linenga alitaja sifa za mwanamke ambaye angependa awe mwandani wake (soma hapa) ambavyo ni “mwenye huruma na maisha yangu, mwenye hofu ya Mungu, anayepata time ya kumuabudu Mungu, anayeniheshimu, anipende mimi sio umaarufu wangu sio pesa zangu” alimaliza Linex.

Bila shaka mrembo huyo atakuwa amekidhi vigezo hivyo kabla ya kupewa usajili na makazi kwenye moyo ya Linex Sunday Mjeda.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW