Michezo
Lionel Messi afutiwa mashtaka ya kukwepa kodi Hispania
Mchezaji wa timu ya taifa Argentina na Barcelona Lionel Messi amefutiwa mashtaka ya kukwepa kulipa kodi ya zaidi ya pauni milioni 4 kwa mamlaka za Hispania. Yeye na baba yake walishtakiwa.
Waendesha mashtaka nchini humo wamefuta mashtaka hayo kwa Lionel Messi lakini wataendelea na kesi dhidi ya baba yake.
Baba yake Lionel Messi, Jorge Messi (katikati)
Kama baba yake atashtakiwa, atakabiliwa na kifungo cha miezi 18 gerezani na faini ya pauni milioni 2.