Michezo

Lionel Messi akutwa na tatizo la figo

Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona Lionel Messi hakuwepo katika mazoezi siku ya Jumatatu ili kupimwa figo yake. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina alikosa kucheza mechi ya nusu fainali ya kilabu bingwa duniani baada ya kupatikana na tatizo la figo,baada ya kuwa na maumivu ya tumbo yanayosababishwa na mawe ndani ya figo.

151006153412_lionel_messi__640x360_epa_nocredit

Taarifa ya kilabu ya Barcelona imesema kuwa Messi mwenye umri wa miaka 28 atarudi katika hali yake ya kawaida siku ya jumatano.
”Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi atafanyiwa vipimo kadhaa Jumatatu na Jumanne ili kubaini hali ya tatizo hilo la figo alilopata mwezi Disemba”,ilisema.

Alicheza dakika 90 siku ya jumapili katika ushindi wa 2-0 dhidi ya kilabu iliopo chini ya jedwali ya Levante.
Siku ya Jumatano ,Barcelona itaitembelea Valencia katika awamu ya pili ya nusu fainali ya Kombe la Copa del Rey ambapo wanaongoza kwa jumla ya mabao 7-0.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents