Michezo

Lionel Messi amgalagaza Cristiano Ronaldo kwenye tuzo za La Liga

Lionel Messi ametajwa kama mchezaji bora na kumpiku Cristiano Ronaldo kwenye tuzo za kila mwaka za La Liga zilizotolewa jijini Barcelona, Jumatatu hii.

Ronaldo-Messi

Tuzo hizo zilizotolewa siku moja ambayo wawili hao pia walitajwa kwenye majina yaliyochujwa kwenye tuzo ya Ballon d’Or ilikuwa moja kati ya mbili zilizochukuliwa na staa huyo wa Argentina.

Naye kocha wa Barcelona, Luis Enrique alitajwa kama kocha wa mwaka.

Messi pia alishinda mshambuliaji bora huku Neymar akishinda mchezaji bora wa Amerika.

Hata hivyo Ronaldo naye alishinda tuzo ya Fans’ Five Star Player huku nahodha wa Madrid, Sergio Ramos akitajwa kuwa beki bora na tuzo ya kiungo bora ikienda James Rodriguez wa Columbia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents