Aisee DSTV!

Lionel Messi ampigia saluti Cristiano Ronaldo ‘Juventus walinishangaza sana, sikuamini’

Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi amemwagia sifa hasimu wake, Cristiano Ronaldo kwa kutupia goli tatu kwenye mchezo kati ya Juventus dhidi ya Atletico Madrid.

Image result for messi
Lionel Messi

Messi amesema kuwa kwenye mchezo huo wa hatua ya 16 bora ambao Juventus alishinda goli 3-0, hakuamini kama Juventus wangefuzu na kudai kuwa ulikuwa usiku wa maajabu kwa Ronaldo, ambaye andiye alitupia goli zote tatu.

Cristiano na Juventus walikuwa vizuri sana (kwenye mchezo wa marudiano kati Juventus vs Atletico). Nilishangazwa na matokeo, kwani niliamini Atletico wangekuwa wagumu lakini Juventus walifanikiwa kuwazidi na Ronaldo akaonesha maajabu yake kwa zile goli tatu.“ameeleza Messi wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari jana usiku baada ya mchezo wa Barcelona dhidi ya Lyon.

Kwenye mchezo huo Messi alitupia goli 2 kati ya 5-1 alizofungwa Lyon na kuifanya Barca kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW