Michezo

Lionel Messi amtaka Mohamed Salah ndani ya Barcelona

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi ameutaka uongozi wa klabu yake ya Barcelona kuhakikisha inanasa saini ya Mohamed Sala kwenye kipindi hiki cha usajili.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun limeeleza kuwa nyota huyo ameutaka uongozi wa klabu hiyo kuhakikisha unamsajili Salah anayekipiga kwenye klabu ya Liverpool ili kuja kujenga muunganiko bora kati yake pamoja na Luis Suarez katika eneo la safu ya ushambuliaji.

Salah mwenye umri wa miaka 26 ametwaa tuzo ya mfungaji bora ligi kuu nchini Uingereza msimu uliyopita nakujiondokea na kiatu cha dhabu baada ya kufunga jumla ya mabao 44 akiitumikia klabu ya Liverpool ndani ya Anfield hivyo kumfanya kulipwa mkwanja mnono wa pauni laki 185,000 kwa wiki.

Mmisri huyo amejiunga na majogooo hao wa Uingereza akitokea Roma ya Italia mwaka 2017 kwa dau dogo la pauni milioni 34.3 lakini sasa thamani yake imefikia pauni milioni 100 kwa klabu yoyote itakayo taka kumng’oa hapo Anfield.

Mabingwa hao wa La Liga klabu ya Barcelona wanatafuta mbadala wa Antoine Griezmann ambaye ameonekana kuhitaji kuendelea kusalia ndani ya timu yake ya Atletico Madrid.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents