Michezo

Lionel Messi aongeza mkataba mpya Barcelona

Mshambuliaji wa klabu ya FC Barcelona na timu ya taifa ya Argentinia, Lionel Messi amesaini mkataba mpya wa miaka minee utakaomuweka ndani ya timu hiyo hadi mwaka 2020/21.

Rais Josep Maria Bartomeu na Lionel Messi wakisaini mkataba asubuhi ya leo siku ya Jumamosi

Messi, amesaini mkataba huo asubuhi ya leo siku ya Jumamosi  ambao utamuweka staa huyo wa Argentinian hadi msimu wa mwaka 2020/21 na kulipwa paundi 500,000 kwa wiki huku kipengele cha ununuzi kikiwa ni euro milioni 700 ili kuepusha yale yaliyojitokeza kwa Neymar wakati alipohitaji kusajiliwa na PSG.

Kwa usajili huo utamfanya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30, kuwa ndani ya klabu hiyo kwa miaka 17

Lionel Messi amejiunga na Barca mwaka 2000 akiwa na umri wa miaka 13 alipo wasili akitokea klabu ya Newell’s Old Boys nchini Argentinian.

Baada ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu na kuvutia katika timu mbalimbali za vijana ndipo akaitumikia timu ya wakubwa kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 16 ukiwa mchezo dhidi ya FC Porto kisha kuanza rasmi kucheza akiwa na umri wa miaka 17 dhidi ya Espanyol.

Leo Messi amekuwa ni mchezaji ambaye anavunja rekodi zilizowahi kuwekwa kilasiku hadi kuwa moja kati ya mchezaji bora katika historia ya soka, kwa kuwa na idadi mengi ya mabao, mataji, rekodi akiwa yeye kama yeye na hata tuzo mbalimbali akiwa na timu yake ya Barcelona.

Messi ameshinda karibu kila kitu, mataji nane ya La Liga, manne ya Champions League, matano ya Copas del Rey, saba ya Spanish Super Cup, matatu ya European Super Cup na mataji mengine matatu ya klabu bingwa ya dunia (Club World Cup). Hivyo jumla amechukua mataji 30, ikiwa sawa na mchezaji mwenzake wa Barca, Andrés Iniesta ambao wote hawa wanaweka historia ya klabu.

Tuzo alizochukua akiwa peke yake, mshindi mara tano wa Ballon d’Or  ikiwa hakuna aliyewahi kufikisha idadi hiyo katika historia ya mchezo wa soka, nne za Pichichi akiwa kama mfungaji bora wa Hispania na tuzo nyingine  nne za kiatu cha dhahabu barani Ulaya.

Ndani ya Barca mchezaji huyo wa Argentina anaevalia jezi namba 10 mgongoni amefunga jumla ya mabao 523 katika michezo 602 aliyocheza ndani ya klabu na Laliga kwa ujumla.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents