Aisee DSTV!

Lionel Messi arudisha matumaini ya Argentina kusonga mbele michuano ya Copa America, Hatma yao ipo mikononi mwa Colombia

Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi jana usiku ameisaidia timu yake ya taifa  kupata matokeo ya sare ya 1-1 dhidi ya Paraguay.

Lionel Messi

Argentina ndiyo iliyosawazisha kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Lionel Messi kunako dakika ya 57 baada ya goli la kwanza la Paraguay kufungwa kunako dakika ya 32.

Kwa matokeo hayo, Argentina itahitaji ushindi kwa hali na mali dhidi ya Qatar. Lakini pia licha ya ushindi huo watahitaji Colombia washinde dhidi ya Paraguay au wapate sare ya namna yoyote ile ili waweze kusonga mbele.

Kwenye msimamo kwa sasa Colombia wamefuzu kwenye hatua ya makundi moja kwa moja baada ya kushinda mechi mbili na ndio wanaongoza kundi hilo.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW