Michezo

Lionel Messi atuma salamu za vitisho kwa timu zinazoshiriki klabu bingwa barani Ulaya

Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi amesema kuwa licha ya umri wake kuwa unasonga mbele lakini anajiona bado mdogo na anazidi kuimarika uwanjani kadri siku zinavyozidi kwenda.

Lionel Messi

Akizungumza kwenye mahojiano yake na mtandao wa klabu hiyo wa fcbarcelona.com amesema kuwa mfumo wa Barcelona bado haujabadilika toka zamani bali kuna ubunifu tu ulioongezeka jambo ambalo linawafanya wachezaji wa klabu hiyo kuwa na furaha uwanjani hata kama matokeo yakiwa ni tofauti.

Kuhusu msimu huu mpya wa Klabu Bingwa barani Ulaya ambao leo usiku mechi za michuano hiyo zinaanza, amewaahidi mashabiki wa klabu hiyo kuwa watarajie kuona kombe hilo likitua Nou Camp kwani ni miaka mingi hawajachukua.

Nadhani tunakikosi kipana na tuna wachezaji wapya, nguvu imeongezeka karibia kila sehemu. huu ni muda wa mashabiki wetu kurudisha furaha kwa kuliona kombe hilo Nou Camp, kama ilivyozoeleka, naahdi tutafanya hivy,“amesema Lionel Messi.

Jana Messi alikuwa anasherehekea miaka 18 tangu mwaka 2000 alipojiunga na klabu hiyo akitokea huko kwao Argentina.

Leo Septemba 18, 2018  klabu ya Barcelona itavaana na PSV kwenye mchezo wa makundi ya kalbu bingwa barani Ulaya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents