Tia Kitu. Pata Vituuz!

Lionel Messi na wengine Barcelona kupimwa ‘CORONA VIRUS’ kabla ya kuwakabili Napoli

Uwepo wa virus vya Corona umeanza kuonyesha athari na kuongezeka kwa hofu katika ramani ya soka, kwenye baadhi ya nchini kadhaa duniani ikiwemo Italia ambayo wiki hii klabu za nchi hiyo zikiwa kwenye michuano ya  Champions League na Europa League.

Image result for Lionel Messi sad moment in barcelona

Siku ya Jumanne Napoli itawakaribisha Barcelona hatua ya 16 bora ya Champions League wakati Inter Milan ikiwa mwenyeji dhidi ya Ludogorets hatua ya 32 michuano ya Europe League siku mbili baadae.

Kwa mujibu wa ESPN, Lionel Messi pamoja na kikosi kizima cha Barcelona watalazimika kufanyiwa vipimo wakati wa kuingia katika nchi hiyo kwenda kucheza na Napoli na hata muda kuondoka hiyo ni kwa mujibu wa Serikali ya Italia.

Kikosi hicho kinasafiri kwenda Kusini mwa Italia Jumatatu hii na lazima kitafanyiwa vipimo vya joto wakati wanawasili uwanja wa ndege wa Napoli-Capodichino airport.

ESPN imefika mbali zaidi na kusema kuwa kama endapo yoyote kati ya wasafiri hao atabainika kuwa kiwango cha juu cha joto basi atachukuliwa na kupelekwa hospitgali moja kwa moja ambapo atakuwa kwenye uwangalizi mkali.

Mlipuko wa coronavirus umeathiri zaidi ya watu 80 nchini Italia huku wawili wakipoteza maisha ikiwa ni sehemu ya visa vilivyowahi kuripotiwa Kaskazini mwa nchi hiyo.

Na siku ya Alhamisi sehemu ya Kaskazini mwa nchi hiyo kutafanyika kwa mtanange wa Europa League wa Inter Milan dhidi ya Ludogorets.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW