Burudani

Lipstick mpya za Rihanna ‘Riri Woo’ zathibitika kumdhuru mmoja wa watumiaji

Tarehe 2 May mwaka huu Rihanna alitambulisha bidhaa mpya ya lipstick ambayo mara baada ya kuingia sokoni stock ya kwanza iliisha ndani ya masaa matatu kutokana na kugombaniwa kama karanga na wateja.

Riri lipstic

Ilikuwa ni moment nzuri kwa Riri kuona bidhaa yake mpya ya ‘Riri Woo’ aliyoshirikiana na kampuni ya Mac imepokelewa vizuri na wateja ambao obviously ni mashabiki wake pia, na kusheherekea kwa kutengeneza keki yenye muundo kama wa lipstick wiki moja baada ya uzinduzi huo.

Riri cake

lakini lipstick hiyo yenye brand yake imekuja kuingia dosari baada ya mwanamke mmoja wa Harlem kulalamika kuwa amedhurika baada ya kuitumia.

Msichana huyo aitwaye Starkeema Greenidge mwenye miaka 28, alisema alipata malengelenge baada ya mwakilishi wa Mac Cosmetics kumpaka lipstick hiyo ya ‘Riri Woo’ ambayo ilikuwa imeshatumika wakati wa show ya Rihanna huko Brooklyn.

Binti huyo aliuambia mtandao wa New York Daily News kuwa “sikuweza kufanya kazi kwa wiki mbili, na imenigharimu pesa nyingi”.

Dr aliyemtibu Greenidge alisema inawezekana kwa mtu kuambukizwa malengelenge kwa kushare lipstick iliyotumiwa na mtu mwenye matatizo hayo na kuongeza kuwa tatizo hilo linaweza kusambazwa na vitu tofauti mbali na lipstick ikiwa ni pamoja na vyombo vya kulia chakula kama vijiko na uma, sigara, miswaki, mabomba ya kuvuta vitu kama shisha na kitu chochote kinachohusiana na kugusa mdomo.

““If someone has an active a cold sore/herpes then yes, it could be transmitted by sharing lipstick”.

Rihanna alisaini deal na kampuni ya Mac mwezi February 2013, kwaajili ya kutengeneza vipodozi vyake kupitia Mac.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents