Habari
Lissu afikishwa Mahakamani Kisutu
Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu anapelekwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusomewa mashtaka yanayomkabili.
Lissu amefikishwa Mahakamani hapo baada ya kulala rumande.
Tundu Lissu alikamatwa Julai 20, 2017 akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam akielekea Rwanda kuhudhuria mkutano wa vyama vya Wanasheria Afrika.
Na Emmy Mwaipopo