Michezo

Listi ya klabu 100 tajiri Afrika yaanikwa, timu mbili zatoka Afrika Mashariki

Kampuni ya ‘Finances of Football’ imetangaza listi ya klabu 100 tajiri barani Afrika huku kila moja ikipangwa kutokana na kipato chake pamoja na matumizi yake.

Makao makuu ya klabu ya Simba yaliyopo mitaa ya Karia Koo
Kwamujibu wa Finances of Football, Afrika Mashariki zimetoa klabu mbili pekee ambazo ni Simba SC ya Tanzania ikiwa nafasi ya 60, huku ikikadiriwa kuwa dola za Kimaarekani 2,230,050 na Gor Mahia kutoka Kenya ikiwa ya 78 ikiwa na kiasi cha dola 1844585.

Kwenye listi hiyo timu ya Al Ahly inaongoza kwa kushika nafasi ya kwanza ikikadiriwa kuwa dola za Kimarekani milioni 28, ikifatiwa na Kaizer Chiefs kutoka Afrika Kusini ikiwa na dola milioni 23 nafasi ya tatu ikishikiliwa na Pyramids wakati ya nne ikienda kwa Club African na ya tano ikishikiliwa na Zamalek yenye dola za Kimarekani milioni 18.and Orlando Pirates.

Hakuna klabu yoyote kutoka Rwanda ,Uganda wala Malawi zilizoingia kwenye listi hiyo wakati TP Mazembe ikiwa ni klabu pekee kutoka Kongo iliyoingia nafasi ya 10.

Kwa mujibu wa Finances of Football listi ya klabu hizo 100 zimepangwa kulingana na akaunti za klabu pamoja na bajeti zao za mwaka kutoka katika vyonza vya kuaminika.

Kikosi cha wachezaji wa Simba

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents