Michezo

LIVE: Mamilioni yaingia Simba, SportPesa watoa pongezi kwa mabingwa wa Nchi (+Video)

Kampuni ya burudani na michezo SportPesa Limited leo Alhamisi tarehe 02 Julai 2020 imekabidhi hundi ya shilingi Milioni 100 kwa Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, timu ya Simba SC

Hafla hiyo ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ofisi za SportPesa ambao ni wadhamini wakuu wa Wekundu hao wa Msimbazi zilizopo maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam, Waliohudhuria kutoka SportPesa ni Mkurugenzi Mtendaji ndugu Pavel Slavkov, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti Tarimba Abbas na Meneja Uhusiano na Mawasiliano Bi. Sabrina Msuya, kutoka Simba ni Mkurugenzi Mtendaji ndugu Senzo Mazingiza, Msemaji Mkuu wa Klabu Haji Manara, benchi la ufundi wakiambatana na wachezaji wote.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa ndugu Tarimba Abbas alianza kwa kuwapongeza wachezaji na viongozi wa Simba kwa kutwaa Ubingwa.

”Awali ya yote nianze kwa kuwapongeza viongozi na wachezaji wa Simba SC kwani mmewapa heshima kubwa wana Msimbazi kote nchini na kubwa zaidi ni heshima mliyotupa sisi kama wadhamini wenu wakuu wa mafanikio makubwa katika kipindi chote cha miaka mitatu.”

Ndg, Tarimba aliendelea kwa kufafanua kuhusu kiasi hicho cha pesa ambacho SportPesa imekabidhi kwa Simba kwa kusema ”Simba imeitendea haki nembo yetu ya SportPesa na kampuni inaamini sisi kuwa wadhamini wakuu imekuwa ni moja ya chachu iliyosababisha Simba Sports Club kuchukua Ubingwa huu.”

”Tunachokifanya leo ni kutimiza moja ya ahadi tulitoa wakati tunasaini mkataba wa udhamini mwaka 2017 kuwa tutatoa bonasi ya shilingi Milioni 100 endapo mojawapo ya timu tunazozidhamini itachukua ubingwa wa Ligi Kuu, hivyo bila shaka timu ni Simba SC.”

Akiongea kwa upande wa Simba SC Mkurugenzi Mtendaji Senzo Mazingiza alianza kwa kusema ”Ushindi upo kwenye damu sisi kama wanasimba na kwa msimu huu tumeweza kuweka historia kwa kuibuka mabingwa wa ligi kuu ikiwa bado tuna mechi sita kuchezwa.”

Moja ya jambo ambalo Simba inajivunia msimu huu ni kuwa na mdhamini kama SportPesa ambaye mbali na udhamini , pia tumekuwa tukishirikiana katika shughuli mbalimbali za kiuongozi.”

Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi Bw. Mohammed Dewji napenda kuwashukuru SportPesa kwa moyo wao wa kutuleta mabadiliko ya soka nchini ambayo sisi kama Simba SC tumeyaona kwa upande wetu na tutaendelea kutoa ushirikiano ili kuboresha mahusiano yetu.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents