Michezo

Liverpool hii ni kali kuliko niliyoipa Ubingwa wa Champions League mwaka 2005 – Benitez

Aliyekuwa kocha wa Liverpool, Rafael Benitez amesema kuwa kikosi cha sasa cha timu hiyo ni bora zaidi ukilinganisha na ile aliyoipatia ubingwa wa klabu bingwa barani Ulaya.

 Aliyekuwa kocha wa Liverpool, Rafael Benitez 

Liverpool wakiwa anajiandaa kuwakabili Real Madrid siku ya Jumamosi iliwahi kufanikiwa kuifunga klabu ya AC Milan hatua kama hiyo na kutawazwa kuwa mabingwa mwaka 2005 huko Istanbul baada ya kutoka nyuma ya mabao 3 – 0 yaliyopatikana kipindi cha kwanza.

kikosi cha sasa cha timu ya Liverpool,  Mohamed Salah, Roberto Firmino na Sadio Mane

“Tulifanikiwa kile tulichofanikiwa licha yakuwa watu waliamini kuwa ni miujiza ndani ya Istanbul lakini ninaamini hii ni timu bora,” amesema Benitez

Meneja huyo amesema kuwa wakati wake alikuwa na wakali kama Steven Gerrard,  Xabi Alonso na Dietmar Hamann wakati kikosi cha sasa cha Jurgen Klopp akiwa nao Mohamed Salah, Roberto Firmino na Sadio Mane.

Salah akiwa amefunga mabao 10, Firmino 10 na Mane tisa yanaifanya safu hiyo kuwa na idadi ya jumla ya mabao 29 kwenye michuano hiyo ya klabu bingwa barani Ulaya jambo ambalo kuonekana kufikisha idadi ya juu mno kwenye ufungaji.

“Sisi tulikuwa na Stevie bila shaka wapo baadhi ya wachezaji walikuwa na uzoefu na kiwango bora kama Alonso na Hamann. Pia tulikuwa na wachezaji waliyofanya kazi kwa juhudi kubwa.” ameongeza Benitez.

Meneja huyo mwenye umri wa miaka 58, kwa sasa anaekinoa kikosi cha Newcastle aliwahi kuifundisha Liverpool kuanzia mwaka 2004 hadi 2010.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents