Michezo

Liverpool ikiifunga Manchester nahama CCM – Haji Manara

Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amesema kuwa ikitokea majogoo wa Uingereza, timu ya Liverpool ikaifunga Manchester United katika mchezo wao wa leo hii wa ligi kuu ya EPL basi ataachana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) nakujiunga na Chama Cha Chauma kinachoongozwa na aliyekuwa mgombea Urais, Hashim Rungwe.

Manara ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Instagram.

Ikitokea Liverpool kuifunga Manchester nahama CCM najiunga na chama cha Hashim Rungwe ..hawatufungi hata kwa bahati mbaya

 

Timu ya Liverpool inatarajiwa kuwa ugenini katika dimba la Old Trafford hii leo siku ya Jumamosi kupambana na vijana wa Jose Mourinho Manchester United mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza.

The Reds wataingia uwanjani huku wakiwa nyuma ya United kwa alama mbili pekee katika msimamo wa ligi na hivyo kushinda kwao watapaa hadi nafasi ya pili na kuwapiku mashetani hao wekundu kwakuwa na jumla ya pointi 63 dhidi ya 62.

Kuelekea katika pambano hilo meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kuwa wanahitaji kuwa sawa kwa asilimia 100 ili kushinda mchezo huo.

Wakati kwa upande Mourinho akisema kuwa watu wengi wamejaa kutoa mawazo tu juu ya kikosi chake licha yakuwa ya kwao yanawashinda.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents