Michezo

Liverpool kuchunguza tuhuma za vurugu dhidi ya Sevilla

Klabu ya Liverpool inafanya uchunguzi kufuatia malalamiko kutoka kwa baadhi ya mashabiki wa timu hiyo kulalamikia Polisi kuwafanyia vitendo vya unyanyasaji wakati wa mchezo wao wa klabu bingwa barani Ulaya dhidi ya Sevilla hapo jana siku ya Jumanne.

Baadhi ya mashabiki wa The Reds walishindwa kuingia Uwanjani kushuhudia mchezo huo baada ya kufanyiwa vitendo vya vurugu, mwenyekiti wa kundi la mashabiki la ‘Spirit of Shankly’, Jay McKenna ameliambia gazeti la Liverpool.

Kupitia mitandao ya kijamii ya twitter mashabiki mbalimbali wameandika namna walivyokosa furaha kwa Polisi hao kwa namna walivyofanya kazi zao katika mchezo huo ambao ulimalizika kwa sare ya mabao 3-3.

Liverpool baada ya kupitia mitandao ya mashabiki imethibitisha leo siku ya Jumatano kuwepo kwa  vitendo visivyo vya kiungwana vilivyokuwa vikifanywa na Polisi katika mchezo wao dhidi ya wenyeji Sevilla.

UEFA imekiambia chombo cha habari cha Sky Sports  kuwa wanafahamu kulikuwa na hali hiyo kwa baadhi ya mashabiki lakini hawana maoni zaidi juu ya hilo kwa wakati huu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents