Michezo

Liverpool kutenga kitita cha fedha kumng’oa Marco Asensio Real Madrid

Klabu ya Liverpool inahusishwa kuhitaji huduma ya kiungo wa Real Madrid, Marco Asensio na hivyo kulazimika kutenga kitita cha pauni milioni 158.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania kwa sasa ameondoka Bernabeu kwaajili ya majukumu ya timu yake ya taifa kwenye michuano ya kombe la dunia huko nchini Urusi.

Liverpool inamkaribisha, Asensio mwenye umri wa miaka 22 kwa mikono miwili Merseyside na kuweka historia ya klabu hiyo kwa kuwa mchezajo atakayelipwa fedha nyingi zaidi Anfield.

Asensio ambaye anajumla ya mabao 11 na pasi sita zilizochangia magoli kwenye kipindi chake cha pili cha msimu wa La Liga huwenda akakabidhiwa jezi namba 10 ambayo ilikuwa ikivaliwa na Philippe Coutinho aliyetimkia Barcelona mwezi Januari.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents