Michezo

Liverpool ndiye bingwa mpya Uingereza – Klopp

By  | 

Meneja  wa klabu ya Liverpool ya nchini Uingereza, Jurgen Klopp amesema kuwa kikosi chake kinaweza kushinda ligi kuu ya nchini Uingereza baada ya kuwa na bahati mbaya msimu uliomalizika.

Meneja  wa klabu ya Liverpool , Jurgen Klopp

Liverpool ambayo ilianza msimu wa 2016-17 katika kiwango bora hali iliyopelekea kuzidiwa alama sita pekee nyuma ya mabingwa klabu ya Chelsea.

Meneja wa klabu hiyo Klopp amesema kuwa ‘Tulikuwa na malengo wakati tunaanza msimu wa ligi, alisema Klopp.

“Ni lazima tuwe na malengo timu yetu ni nzuri sana licha yakuwa na bahati mbaya katika msimu uliomalizika, nadhani tunaweza kucheza vyema. Tuwe na matumaini kuwa kila kitu kitakwenda sawa.

Klop ambaye anaonekana kuwa na wakati mzuri katika klabu hiyo ukilinganisha na watangulizi wake waliopita amesisitiza mchezaji wao raia wa Brazili, Phillipe Coutinho hauzwi licha ya Barcelona kumtaka.

By Hamza Fumo

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments