Michezo

USAJILI: Liverpool waitosa Barcelona

Klabu ya Liverpool imekataa kumuachia mshambuliaji wake, Philippe Coutinho kwenda Barcelona kwa dau la Euro milioni 90.

Tokeo la picha la phillipe coutinho
Philippe Coutinho

Dili la Euro milioni 90 ni la pili kukataliwa baada ya vijogoo hao wa Anfield, Liverpool kuwachomolea dili la kwanza la Euro milioni 76.

Hata hivyo mbio za Klabu ya Barcelona za kutaka kunasa saini ya Coutinho (25) huenda zikaishia njiani kwani klabu ya Liverpool tayari imeshatangaza kuwa haina mpango wa kumuuza mshambuliaji huyo msimu huu.

SOMA ZAIDI Barcelona yathibitisha kuondoka kwa Neymar

Klabu ya Barcelona inahaha kutafuta mchezaji mbadala wa Neymar Jr ambaye amehama klabuni hapo na kujiunga na matajiri wa Ufaransa, PSG kwa dau la Euro milioni 222 na kuweka rekodi ya mchezaji wa mpira ghali zaidi kununuliwa duniani.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents