Michezo

Liverpool yarejea kileleni,EPL baada ya kuichapa Spurs 4-0

Majogoo wa London, Liverpool jana wamejikita kileleni kwenye ligi kuu ya Uingereza baada ya kuinyuka Tottenham hotspurs mabao 4-0 katika mechi iliyokuwa ikisubiriwa na wengi iliyochezwa uwanjani wa Anfield.

Liverpool's Luis Suarez celebrates after scoring during their English Premier League soccer match against West Ham United at Anfield in Liverpool, northern England December 7, 2013. REUTERS/Phil Noble (BRITAIN - Tags: SPORT SOCCER) FOR EDITORIAL USE ONLY. NOT FOR SALE FOR MARKETING OR ADVERTISING CAMPAIGNS. NO USE WITH UNAUTHORIZED AUDIO, VIDEO, DATA, FIXTURE LISTS, CLUB/LEAGUE LOGOS OR "LIVE" SERVICES. ONLINE IN-MATCH USE LIMITED TO 45 IMAGES, NO VIDEO EMULATION. NO USE IN BETTING, GAMES OR SINGLE CLUB/LEAGUE/PLAYER PUBLICATIONS - RTX168E7

Younes Kaboul alijifunga mwenyewe kunako dakika ya pili baada ya pasi ya chini kwa chini kutoka kwa Glen Johnson na baada ya hapo Luis Suarez alifunga bao la pili baada ya mchezaji wa Spurs kucheza visivyo. Philippe Coutinho alirudi tena kwenye nyavu za Tottenham kwakupachika bao la bao la tatu.

Jordan Henderson alifunga bao la nne kwa mkwaju wa free-kick. Ushindi huo sasa umeifanya Liverpool kurejea kileleni kwa alama 71, mbili zaidi ya wapinzani wao wa karibu Chelsea. Liverpool wanaiongoza Manchester City kwa alama nne licha ya vijana hao wa Manuel Pellegrin kuwa na mechi mbili zaidi za kucheza. Hata hivo Man City na Chelsea bado watakabiliana na vijana wa mkufunzi Brendan Rodgers Liverpool katika uga wa Anfield.

Iwapo watashinda mechi hizo basi Liverpool itajiweka katika nafasi nzuri ya kunyakua taji la ligi kuu kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1989-90.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents