Habari

LL Cool J amfundisha adabu jambazi aliyevamia nyumbani kwake



Rapper na muigizaji wa filamu LL Cool J jana alfajiri alijikuta akiigiza filamu ya ukweli baada ya kumtandika vilivyo jambazi aliyevamia nyumbani kwake.
Kwa mujibu wa vyanzo, jambazi huyo aliingia mida ya saa 8 usiku kwenye nyumba yake ya Los Angeles lakini bahati mbaya muigizaji huyo aliyejazia alikuwa ndani.
Inadaiwa kuwa Cool J James ambaye jina lake halisi ni James Todd Smith alisikia vishindo chini ya nyumba yake eneo la jikoni na kuamka kushuka kuangalia ambapo alimkuta mwizi huyo akijiandaa kuchukua mali kama za kwake vile.
Kutokana na kuwa fit katika sanaa ya mapigano, LL alimwangushia kichapo heavy mwizi huyo na kumpasua pua, mbavu na taya.
Baada ya polisi kuwasili kwenye eneo la tukio walimkuta mhalifu huyo akiwa ametepeta kama uji na akivuja damu usoni ambapo baadaye alikuja kubainika kuwa ni Jonathan Kirby, 56, aliye na rekodi za matukio mbalimbali ya wizi, kupigana na matumizi ya madawa ya kulevya.
Katika mapigano hayo msanii huyo hakujeruhiwa sehemu yoyote.
Rekodi za mahakama zinaonesha kuwa Kirby aliwahi kuhukumiwa kifungo cha miaka mitano kutokana na ujambazi miaka ya 1990 na miaka mitatu kwa wizi wa kawaida.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents