Michezo

Logarusic ametagazwa kuwa kocha mpya wa klabu hii ya Ghana

Kocha wa zamani wa klabu ya Simba, Mcroatia, Zdravko Logarusic, ametagazwa kuwa kocha mpya wa klabu ya Asante Kotoko ya Ghana amesaini mkataba wa miaka miwili kuinoa timu hiyo baada ya kuachana na klabu ya Interclube ya Angola.

Logarusic ambaye aliifundisha Simba kuanzia Desemba, 2013 mpaka Julai, 2014, Novemba mwaka jana alimaliza mkataba wa kuifundisha kalabu ya Interclube huku akifanikiwa kuipa kombe la chama cha soka la nchi hiyo, APFL.

Mtandao wa habari za michezo wa nchi ya Ghana wa Soccernet, jana Jumanne uliripoti kuwa:

“Asante Kotoko imeingia mkataba wa miaka miwili na kocha raia wa Croatia, Zdravko Lugarusic, ataanza kuinoa timu hiyo ndani ya wiki hii baada ya kukamilisha taratibu za kupata kibali cha kazi.”

Ni mudasasa timu ya Asante Kotoko ilikuwa haina kocha mkuu tangu Machi, mwaka jana baada ya aliyekuwa kocha wao, David Duncan kuachia ngazi kutokana na matokeo mabaya aliyokuwa akiyapata. Kwa muda wote huo, kikosi hicho kilikuwa chini ya kocha msaidizi, Michael Osei.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents