Burudani

Lollypop adai bado hajaifanya kazi ya kuandikia wasanii nyimbo kuwa rasmi

Mtayarishaji wa muziki na mtunzi wa nyimbo, Lollypop, amesema bado hajaamua kuifanya kazi ya kuwaandikia wasanii nyimbo kuwa rasmi.

Lollipop

Akizungumza katika kipindi cha 5T40 cha Radio 5 ya Arusha, Lollypop alisema wasanii wengi aliofanya nao kazi ni watu wake wa karibu.

“Mimi kuandika kwanza sio kazi official, huwa naandika kuna situation zinatokea na zinanibidi niandike na naandika na watu ambao tuko close sana,” alisema. “Haitokeagi tu nakaa naanza kuandika nyimbo mtu anakuja ananilipa tunafanya. Kwa mfano kwa habari ya Mo Music nimekuwa naye, nimekaa naye street moja ni watu ambao tumekuwa pamoja,” aliongeza.

“Kwahiyo nilifanya kwa sababu ni ambaye tulikuwa close. Pia kwa Barakah nimekuwa na mahusiano ya karibu na meneja wake ambaye pia ni producer, kwahiyo huwa kuna sababu ambayo itanifanya ili niweze kufanya kazi na mtu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents