Habari

Lord Eyez ampa ushauri Ommy Dimpoz, adai kuna uwezekano wa kuwepo filamu ya Mapito

Ikiwa ni siku kadhaa tu tangu Lord Eyez aachie wimbo wake mpya, Mapito, rapper huyo ameibuka na kumpa ushauri muhimu Ommy Dimpoz.

http://www.youtube.com/watch?v=EDqPXvbXqBY&list=UUrJ5CGMLyFFLnKtVNpgxtrQ&index=5

Akiiambia website ya Leotainment, Lord Eyez amemwambia Ommy Dimpoz kuwa auheshimu muziki kwakuwa ndio unaomlisha.

“Halafu aheshimu kila mtu manake hajui ni nani aliyempandisha na nani atakayemshusha na asichukulie kitu for granted, asichukulie jina la mtu ama akachukulie mtu kama ngazi ya kumfikisha sehemu fulani, uwe unaangalia ukweli, ” amesema Lord Eyez.

“Manake Ommy Dimpoz alifaa aiambie Tanzania kwamba mimi sina Kesi na Lord na wala sijamfungulia kesi, manake gari langu limefanyiwa hivi na hivi lakini mwizi nimeshamjua lakini sio Lord. Na kitu kingine ni kwamba mimi kesi sasa hivi sina kwa sababu kesi zote zilikuwa za uzushi, ndo maana sikufika hata magereza niliishia polisi nikapelekwa mahakamani nikadhaminiwa na kesi hazikuwa hata na mlalamikaji ni kesi za kizushi kwa hiyo zikafutwa zote.”

Pia Lord Eyez amefunguka kuwepo uwezekano wa filamu ya wimbo wake, Mapito.

“Na kwa habari za juu juu tu ni kwamba kunaweza kukapatikana filamu ya hiyo ngoma manake kuna madirector wamenifata wamenambia yaani huu wimbo sio wa kupita tu hivi hivi sisi tunataka kufanya filamu yake..kwa hiyo inakuja filamu based on true story, vitu vingi vitakavyoonekana kwenye hii movie vitakuwa ni ukweli mtupu, na mhusika ni mimi mwenyewe Lord Eyez.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents