Habari

Lord Eyez Kufungua Milango ya Nako 2 Nako.

Lord Eyez“Ni mwanajeshi toka pande za North hakunaga mwingine” ni maneneo yake msanii na kiongozi wa kundi la Nako 2 Nako Lord Eyez ambaye anatarajia kujikata na kuelekea nchi kadhaa za ulaya kwa ajili ya kufanya maonesho

Lord eyez


“Ni mwanajeshi toka pande za North hakunaga mwingine” ni maneneo yake msanii na kiongozi wa kundi la Nako 2 Nako Lord Eyez ambaye anatarajia kujikata na kuelekea nchi kadhaa za ulaya kwa ajili ya kufanya maonesho na hili atalifabikisha mara atakapomaliza kukamua kwenye show ya tarehe 28 Leaders Club mwishoni mwa mwezi huu.


Akizungumza na mwandishi wa Bongo5 alisema “natarajia kutimba nchi kibao lakini nyingine ni kwa ajili ya matembezi na shughuli zangu za kisanii ila nitapiga show Uingereza, Norway na Netherlands na kuna manchi kibao yanahitaji nikapige show lakini bado hatujaafikiana kimkwanja”-Lord Eyez.


Katika safari hiyo anatarajia kuongozana na mamsapu wake ambaye nae ana ziara katika nchi 12 tofauti ikiwepo marekani, huyu si mwingine bali ni Binti Kiuno a.k.a Ray 2 Tha C jina halisi Rehema ‘Ray C’ Chalamila, mmoja kati ya wasanii wa kibongo wanaopiga sana vimeo katika nchi za watu. “katika vitu ambavyo sitaacha kuvifanya mara nitakapotua nitamtafuta mtu mzima ZiggyLah wa kundi la X-Plastaz kwa ajili ya kupiga nae mikono kadhaa kwenda kuifungua milango ya WaNako”.


Jamaa hao ambao wanakomaa na kuitangaza albam yao inayokwenda kwa jina la ‘hawahemi streets hustler’ Vol 1 ambayo inapatikana mitaani hivi sasa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents